Mamia Ya Wanafunzi Waliotekwa Nigeria Waachiwa Huru

 

Mamia ya wavulana waliotekwa wiki iliyopita kutoka shule ya bweni kaskazini -magharibi mwa Nigeria wameachiliwa huru, mamlaka katika eneo hilo zimeambia BBC.

Msemaji wa gavana wa jimbo la Katsina amesema wavulana 344 wameachiliwa huru na kwamba wako katika hali nzuri.

Hata hivyo, ripoti zingine zinaashiria kuwa baadhi yao wamesalia mikononi mwa watekaji wao.

Shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa na na wanamgambo la Boko Haram, ambalo awali lilitoa video ikiwaonyesha baadhi ya wavulana hao. Katika taarifa yake, msemaji, Abdul Labaran, amesema wavulana hao walikuwa wakipelekwa katika mji mkuu wa mkoa wa Katsina, na hivi karibuni wataungana na familia zao.

Amesema video iliyotolewa na na Boko Haram ilikuwa ya kweli, lakini ujumbe unaonekana kutoka kwa kiongozi wa kikundi hicho Abubakar Shekau, ulikuwa wa kuiga.


EmoticonEmoticon