Marekani, China Zaendelea Kudhibiti Soko La Silaha

Ripoti mpya ya taasisi ya kimataifa ya utafiti wa amani SIPRI yenye makao yake mjini Stockholm, SIPRI imeonyesha kuwa makampuni ya silaha ya China na Marekani yalilidhibiti soko la silaha ulimwenguni kwa mwaka 2019. 

Lakini pia ripoti hiyo imesema Mashariki ya Kati kwa mara ya kwanza imeingia kwenye orodha ya wazalishaji wakubwa zaidi 25 wa silaha ulimwenguni.

Kulingana na ripoti ya SIPRI, makampuni ya Marekani na China ndio yaliyolikamata soko la silaha kwa mwaka 2019, wakati Mashariki ya Kati ikijitokeza kwa mara ya kwanza miongoni mwa vigogo 25 wa kuzalisha silaha ulimwenguni.

data zilizochapishwa na SIPRI hii leo zimeonyesha makampuni ya silaha yaliyojikita nchini Marekani yalichukua nafasi tano za mwanzo mwaka jana, wakati kampuni ya Lockheed Martin, Boeing, Northrop Grumman, Raytheon na General Dyanamics yakifanya biashara ya dola bilioni 166 katika  mauzo jumla ya mwaka.

Kwa ujumla, makampuni 12 ya Marekani yamekuwa miongoni mwa makampuni hayo 25 makubwa zaidi yanayozalisha silaha, na kufanya asilimia 61 ya mauzo jumla ya silaha.

EmoticonEmoticon