Marekani imesema kundi la waasi linaloendesha oparasheni zake kaskazini mwa Msumbiji lina mafungamano na wapiganaji wa kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu - IS.
Vyanzo vya kijeshi vimeliambia
shirika la habari la AFP kuwa mapema wiki hii, wapiganaji wa kundi hilo la
kijihadi linalojulikana kama Ahlu Sunna Wa-Jamaa walishambulia kijiji kimoja
kaskazini mwa Msumbiji karibu na sehemu kunakoendeshwa mradi mkubwa wa gesi.
Marekani imesema waasi hao wana mafungamano na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu, na imeahidi kuisaidia serikali ya Msumbiji kukabiliana na kundi hilo.
EmoticonEmoticon