Marekani Yaidhinisha Chanjo Ya BioNTech-Pfizer

 

Idara ya Chakula na Madawa nchini Marekani, FDA imeiidhinisha chanjo ya virusi vya corona ya kampuni ya BionTech na Pfizer kwa ajili ya kutumika nchini humo. 

Mwanasayansi mkuu wa FDA, Denise Hinton amemuandikia barua mkurugenzi wa Pfizer kumueleza kwamba anaidhinisha chanjo hiyo kwa matumizi ya dharura. Chanjo ya kwanza inatarajiwa kutolewa kwa wahudumu wa afya na wazee wanaoishi kwenye nyumba maalum za kuwaangalia wazee. 

Kamati ya ushauri ya Vituo vya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Marekani, CDC inatarajiwa kupendekeza nani atakayekuwa wa kwanza kupatiwa chanjo hiyo. 

Waziri wa Afya na Huduma za Binaadamu, Aley Azar amekiambia kituo cha televisheni cha ABC News kwamba serikali ya Rais Donald Trump ilikuwa ikishirikiana na Pfizer kuhusu suala la usambazaji na huenda wakashudia watu wakipewa chanjo hiyo Jumatatu au Jumanne ijayo.


EmoticonEmoticon