Marekani Yaidhinisha Chanjo Ya Pili Ya Corona

 

Moderna imeidhinishwa na serikali ya Marekani kama chanjo ya pili ya corona nchini humo, baada idhini ya kusambazwa kwa dozi za chanjo hiyo kutolewa.

Mamlaka ya kusimamia usalama wa chakula na dawa (FDA) iliidhinisha chanjo hiyo iliyongenezwa Marekani karibu wiki moja iliyopita baada ya kuidhinisha chanjo ya Pfizer/BioNTech ambayo kwasasa inatolewa.

Marekani ilikubali kununua dozi milioni 200 ya Moderna, na milioni sita kati ya hizo huenda ziko tayari kusafirishwa.

Nchi hiyo ina idadi ya juu zaidi ya vifo vilivyotokana na ugonjwa wa corona na hali kadhalika viwango vya juu vya maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.

Imerkodi zaidi ya vifo 313 na karibu maambukizi milioni 17.5, kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Kamishena wa FDA Stephen Hahn amesema kuidhinishwa kwa dharura kwa chanjo hiyo siku ya Ijumaa kunaashiria ''hatua nyingine muhimu katika juhudi za kukabiliana na janga la kimataifa ".


EmoticonEmoticon