Umoja wa
Mataifa umesema kuwa mataifa mengi huenda yakachelewa kuwasilisha ripoti kuhusu
udhibiti wa hali ya hewa mwaka huu, kama inavyohitajika kuambatana na mkataba
wa Paris kutokana na janga la corona linaloendelea.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, katibu mkuu wa
Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wiki iliopita alihimiza umuhimu wa kulinda
hali ya hewa akisema wanadamu wako kwenye hatari ya kuangamiza mazingira.
Kwenye mkataba wa Paris uliotiwa saini 2015, mataifa
yalikubaliana kudumisha viwango vya joto chini ya nyusi 2 Celcius, wakati
shirika la Umoja wa Mataifa la UNDP, likisaidia mataifa 115 kati ya 197
yaliotia saini mkataba huo kuhakikisha kuwa hali ya heya inadhibitwa, mengi
yakiwa maskini.
Mataifa hayo yanachangia karibu robo moja ya gesi inayotokana
na greenhouse ulimwenguni yakiwemo Mexico na Nigeria. UNDP hata hivyo limesema
kuwa huenda janga la Covid-19 likawa kizingiti cha mataifa mengi kuwasilisha
ripoti zao kwa wakati.
Kufikia sasa, ni mataifa 8 pekee yalioko chini ya program ya UNDP, ambayo yamewasilisha ripoti zao yakiwemo Rwanda na Mongolia.
EmoticonEmoticon