Mataifa
wanachama katika shirika la umoja wa mataifa linalosimamia dawa, nusra yapigie
kura hatua ya kuondoa vizuizi dhidi ya matumizi ya bangi ili kurahihisha
utafiti kuhusu mmea huo kwa matumizi ya tiba.
Mkutano wa kila mwaka kuhusu dawa za kulevya, ambao huleta
Pamoja maafisa wa umoja mataifa kuhusu dawa na tume inayosimamia uchunguzi wa
uhalifu, wamepiga kura jumatano.
Kura 27 zimepigwa kupinga hatua hiyo huku 25 wakiunga mkono.
Mtu mmoja aliamua kutopiga kura ya kutaka bangi kuondolewa katika orodha ya
dawa za kulevya kulingana na maamuzi namba 4 ya mwaka 1961 ya umoja wa mataifa
kuhusu matumizi ya dawa.
Upigaji kura unafuatia maamuzi ya mwaka 2019 ya umoja wa
mataifa kwamba bangi inastahili kufanyiwa majaribio ya kimaabara na utafiti
kujua kama inaweza kutumika na madaktari kama tiba.
Kulingana na shirika la afya duniani bangi haina madhara
makubwa kiasi cha kusababisha kifo na kwamba imeonyesha uwezo mkubwa katika
kutibu magonjwa kama kifafa.
Taarifa ya umoja wa mataifa haijasema nchi ambazo zimeunga mkono wala kukataa matumizi ya bangi kwa utafiti wa tiba wakati wa kikao hicho cha Vienna.
EmoticonEmoticon