Mamlaka
nchini Afrika Kusini imetoa onyo kwa migahawa kutumia mbinu mbalimbali kuuza
pombe na kukiuka marufuku ambayo imeweka hivi karibuni kufuatia ongezeko la
maambukizi ya Covid 19.
Waziri wa
Polisi, Bheki Cele, amesema migahawa itakayokiuka agizo itanyang’anywa leseni
na wamiliki kufunguliwa mashtaka.
Cele ameionya
migahawa hiyo na kuitaka kutoweka pombe kwenye chupa za chai au zile
zilizoandikwa hakuna kilevi akisisitiza wanafahamu mbinu hizo zote.
Awali, Rais
Cyril Ramaphosa alisema vitendo vinavyotokana na unywaji pombe vimechochea
hatari ya mlipuko kuendelea kusambaa katika nchi hiyo ambayo hivi karibuni
imeripoti aina mpya ya Kirusi cha Corona.
Afrika Kusini
ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya Virusi vya Corona na hivi
karibuni ilirejesha baadhi ya vizuizi kutokana na hali kuwa mbaya tena.
Hadi sasa tayari Afrika Kusini imeripoti visa zaidi ya Milioni moja ambapo kati ya hao zaidi ya watu 850,000 wamepona na wengine zaidi ya 27,000 wamefariki dunia.
EmoticonEmoticon