Messi Avunja Rekodi Ya Pele Kwa Ufungaji Wa Magoli

 

Lionel Messi aliifungia bao lake la 644 Barcelona wakati wa ushindi wa timu hiyo dhidi ya Real Valladolid na kuvunja rekodi ya Pele ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao zaidi katika klabu moja.

Mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka , 33, alifunga bao la Barcelona la tatu alimchenga mlindalango Jordi Masip.

Messi alifunga goli lake la kwanza wakati chenga lake lilipokatizwa na Clement Lenglet na akaanza upya harakati zake kwa ajili ya bao la pili, ambalo lilimaliziwa na Martin Braithwaite.

Mchezaji maarufu wa Brazil ukipenda great Pele alifunga mabao 643 katika misimu 19 katika klabu ya Santos nchijni mwaka baina ya 1956 na 1974.

Messi, ambaye aliifungia goli la kwanza Barca mwaka 2005 aliendelea na kushinda mabao 10 na kupata mataji ya La Liga na manne ya Championi Ligi, sasa mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na anaweza kuongea na klabu nyingine kuanzaia Januari.


EmoticonEmoticon