Mfahamu Nyoka Mwenye Macho Matatu Aliyegunduliwa Huko Australia

 

Maafisa wa wanyama pori walisambaza picha za nyoka mwenye macho matatu aliyepatikana katikati ya barabara kaskazini mwa Auustralia.

Shirika la huduma kwa wanyama pori na bustani za wanyama Northern Territory Parks and Wildlife Service wameeleza kwamba nyoka huyo ambaye picha zake zilisambaa pakubwa katika mitando ya kijamii, ni wa "kustaajabisha".

Alipewa jina la Monty Python, hatahivyo nyoka huyo aina ya chatu alifariki wiki kadhaa tu baada ya kugunduliwa .

Wataalamu wanasema jicho la tatu la nyoka huyo lililo juu ya kichwa chake limeonekana kuwa ni mabadiliko ya asili. Maafisa walimgundua nyoka huyo katika mji wa Humpty Doo, 40km kusini mashariki mwa Darwin.

Ana urefu wa 15 inchi na alikuwa akipata tabu kula chakula kutokana na ulemavu wake, maafisa wameiambia BBC.


EmoticonEmoticon