Mshirika Mkuu Wa Trump Avunja Ukimya Na Kumpongeza Biden

 

Afisa wa ngazi ya juu wa chama cha Republican cha Donald Trump, na kiongozi wa wengi katika bunge la Seneti nchini Marekani-Mitch McConnell, amempongeza Joe Biden kwa ushindi wake katika uchaguzi wa urais mwezi uliopita.

Senata McConnell alizungumza baada ya wajumbe wa uchaguzi -electoral college kuidhinisha rasmi ushindi wa Bw Biden dhidi ya Trump.

Mdemocrat alishinda kura za wajumbe 306 dhidi ya Trump ambaye alipata kura 232.

Rais Trump bado hajakubali kushindwa, na amekuwa akiendelea kutoa madai yasiyo na ushahidi ya wizi mkubwa wa kura.


EmoticonEmoticon