Mtandao Wa Twitter Kuwafuta Wafuasi Wa Donald Trump Kabla Ya Kumkabidhi Mamlaka Joe Biden

 

Twitter imethibitisha kwamba mamilioni ya wafuasi wa akaunti rasmi ya rais wa Marekani watafutwa kabla ya akaunti hiyo kukabidhiwa utawala wa rais mteule Joe Biden.

Timu ya bwana Biden 'iliping'a mpango huo huo lakini kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii ilisema kwamba uamuzi wake 'haubadiliki'.

Hatua hiyo inaashiria mabadiliko kutoka kwa utawala unaoondoka. Twitter ilikubali ombi la rais Donald Trump 2016 kuwarithi mamilioni ya wafuasi wa Barrck Obama.

''Mwaka 2016, utawala wa rais Trump uliwarithi wafuasi wote wa rais Obama katika akaunti ya @POTUS na ile ya @Whitehouse'', Rob Flaherty, mkurugenzi wa masuala ya mtandaoni alisema katika ujumbe wake wa Twitter siku ya Jumatatu.


EmoticonEmoticon