Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye anawania muhula wa sita madarakani, amesema kwamba hajaona mtu mwenye uwezo wa kuongoza Uganda kwa sasa, na hivyo ataendelea kuwa madarakani kwa sababu wapiga kura nchini humo bado wanamhitaji kuendelea kuongoza taifa hilo.
Akihutubia viongozi wa chama chake cha National Resistance Movement (NRM) katika wilaya ya Lukungiri, ambayo ni ngome ya kisiasa ya aliyekuwa mpinzani wake mkuu mara nne Dr. Kiiza Besigye, Museveni amesema kwamba wapinzani wake ni watu wazembe wanaotaka kusukumwa kama mkokoteni.
“Wanajua lengo langu katika siasa
lakini wanataka kunishawishi niache msimamo wangu. Wanapiga kelele kwamba
nastahili kuondoka madarakani utadhani sina pa kwenda,” amesema Museveni
akitumia mojawapo ya lugha zinazozungumzwa magharibi mwa Uganda.
Akiwataja
watatu hao ambao walikuwa marafiki wake wa muda mrefu na mmoja alikuwa daktari
wake binafsi (Dr. Kiiza Besigye), kuwa watu “wasiokuwa na maana yoyote na ambao
sasa wanataka aondoke madarakani.”
Amesema
kwamba "huwa nakasirika sana ninaposikia watu wakiniambia kwamba niondoke
madarakani, lakini huwa najaribu sana kujizuia na kuwa mtulivu.”
“Kama ulishindwa kufanya nilichokuambia, usilete vurugu kwa kuniambia kwamba niondoke madarakani. Wapiga kura ndio wanaoamua,” amesema Museveni akiongezea kwamba “hata nikiondoka nani hao wasiokuwa na maana yoyote ambao wanataka kusukumwa kama mkokoteni wanaotaka kuongoza nchi hii.
Muniache niendelee kuongoza kwa sababu raia wa Uganda wananihitaji niwepo. Nitaondoka tu iwapo kuna mtu wa maana nitakayeona naweza kumuachia Uganda. Nataka niwe na uhakika mahali naiacha Uganda”
EmoticonEmoticon