Mwandishi wa
habari, Raia wa China ambaye amekuwa akizuiliwa gerezani tangu mwezi wa tano
kwa kuonyesha moja kwa moja kupitia mtandao wa kijamii, mlipuko wa virusi vya
Corona katika mji wa Wuhan, amehukumiwa kifungo cha miaka 4 gerezani.
Hukumu yake
imekuja mwaka mmoja baada ya mlipuko wa virusi hivyo ambavyo mwanzoni vilikuwa
vinatajwa kuwa homa ya mapafu.
Zhang Zhan,
ambaye alikuwa wakili, ameshutumiwa kwa kile kimetajwa kama kuanzisha ugomvi na
kusababisha shida, kwa kuripoti kuhusu virusi hivyo wakati vilipolipuka mjini
Wuhan.
Ripoti zake
za moja kwa moja za video na maandishi, zilisambaa sana kwenye mitandao ya
kijamii mwezi Februari.
Maafisa
nchini China wamewaadhibu watu kadhaa waliotoa habari kuhusu kuwepo kwa virusi
hivyo, katika hatua ya kunyamazisha wakosoaji wa serikali namna
ilivyoshughulikia mlipuko wa virusi vya Corona.
Beijing
imejisifu sana kwa kile imetaja kama kufanya kazi kubwa kupata mafanikio
makubwa katika kukabiliana na virusi vya Corona ndani ya mipaka yake.
Imesema
kwamba uchumi wake umeanza kukua.
Nchi zingine
zinapitia wakati mgumu sana kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.
China imechukua katua kali kuzuia usambasaji wa habari kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo.
EmoticonEmoticon