Mwigizaji Tommy Lister maarufu
‘Tiny’ amefariki dunia, imeripotiwa kwamba alikutwa akiwa na hali mbaya kwenye
apartment aliyokua anaishi na kuwaishwa Hospitali alikofia.
Polisi wa Los Angeles wamesema Marafiki zake walipatwa na
wasiwasi kwa ukimya wake toka walipoachana nae siku ya Jumatano na baadae
walivyofatilia wakakuta amefariki.
Pamoja na kwamba utafanyika uchunguzi, Polisi wamesema
wanaamini kifo chake ni cha kawaida na hawadhani kama aliuwawa.
Lister amecheza kwenye movies mbalimbali ikiwemo za FRIDAY
akitumia jina la Deebo, amefariki akiwa na umri wa miaka 62.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon