Nchi Zaidi Zapiga Marufuku Ndege Kwenda Uingereza

 

Nchi zaidi duniani zimeendelea kutangaza kuzipiga marufuku ndege zao kwenda Uingereza ili kuzuia kuenea kwa aina mpya ya virusi vya corona vilivyogunduliwa nchini humo. 

Nchi zilizojiunga na orodha na mataifa kadhaa ya Ulaya ni pamoja na Kuwait, Tunisia, Urusi, Oman, Saudi Arabia pamoja na Chile. Nchi nyingine ni Israel, El Salvador, Morocco, India, Jordan na Argentina. 

Mbali na Uingereza, nchi hizo zimezuia pia ndege kutoka na kwenda Afrika Kusini na Denmark, ambako kuna virusi vipya vilivyogundulika. 

Wakati huo huo, mchambuzi wa kujitegemea wa Uingereza, Dokta John Campbell ameiambia DW kwamba aina mpya ya virusi vya corona vilivyogunduliwa Uingereza huenda vikaambukiza zaidi kwa asilimia 70. Aidha, amesema sababu virusi hivyo vimekuwepo tangu mwezi Septemba, kuna uwezekano tayari vimeingia kwenye nchi kadhaa za Ulaya.


EmoticonEmoticon