Hebu
fikiria, mmeishi kwenye ndoa kwa miaka 24, baadae unagundua kuwa watoto watatu
kati ya wanne ambao umekuwa ukiwalea pamoja na mke wako si wako.
Katika tukio
hilo lililotokea nchini Kenya, shuhuda ambaye ni rafiki wa karibu wa bwana
huyo, Julius Mmasi amefichua kuwa rafiki yake huyo wa karibu amelazimika
kuvunja ndoa hiyo iliyodumu kwa miaka 24.
Hatua hiyo
imekuja baada ya matokeo ya DNA kubainisha kuwa ni baba halisi wa mtoto mmoja
pekee kati ya wanne ambao aliwalea pamoja na mke wake.
Jambo la
kuhuzunisha zaidi ni kuwa mke wake amekiri kuwa bosi wake ndiye baba ya watoto
watatu wa kwanza.
Kwa mujibu wa
Mmasi, rafiki yake huyo aliamua kufanyia watoto wake wanne uchunguzi wa DNA
baada ya kuanza kumshuku mke wake.
Baada ya
uchunguzi huo aligundua kuwa mabinti wake watatu ni watoto wa bosi wa mke wake
huku kitinda mimba ambaye ni wa kiume ndiye mtoto wake pekee halisi katika ndoa
hiyo.
“Watoto watatu wa kwanza wa kike, wawili walifuzu mwingine yuko kidato cha nne. Mke wake alikiri kuwa watoto watatu wa kwanza ni wa bosi wake. Utamshauri mtu kama huyu vipi kuhusu haya?, ndoa ya miaka 24 imevunjika ghafla, maana kuwa wanaume wengi wakiamua kuchukua hatua hii ndoa nyingi zitavunjika” Mmasi.
EmoticonEmoticon