Nyumba Ya Michael Jackson Yauzwa Kwa Mabilioni

 

Nyumba aliyokuwa akiishi mfalme wa muziki wa Pop duniani, marehemu Michael Jackson, imeuzwa kwa bilionea Ron Burkle kwa Dola za Marekani mil. 22 ambazo ni sawa na bil. 51 za Tanzania.

Burkle, ambaye alikuwa rafiki wa zamani wa Jackson, hivi karibuni aliinunua nyumba hiyo iliyoko Los Olivos, California, Marekanim ambapo msemaji wake alisema nyumba hiyo imejengwa katika shamba lenye ekari 2,700 .

Mwanamuziki huyo alilinunua jumba hilo mwaka 1987, wakati ambao alikuwa anafanya vizuri kwenye muziki wa Pop kupewa jina la Mfalme wa Pop.

Alibadilisha jumba hilo na kuwa eneo la burudani, akijenga eneo la kufuga wanyama mbali na ukumbi wa chini ya ardhi ambapo aliwafurahisha watoto na familia zilizokuwa zinamtembelea.


Miaka 1990 hadi 2005, jumba hilo lilichunguzwa sana kutokana na madai ya udhalilishaji watoto kingono dhidi ya mfalme huyo wa Pop.

Jackson hakurudi tena katika kasri hilo na miaka minne baadaye mwezi Juni 2009, alifariki katika nyumba yake nyingine mjini Los Angeles, baada ya kukumbwa na mshtuko wa moyo uliotokana na kunywa dawa kupitia kiasi.


EmoticonEmoticon