Rais Steinmeier: Hali Ni Ngumu Lakini Ujerumani Itashinda

 

Rais Frank-Walter Steinmeier wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani ametumia hotuba yake ya kheri za Krismasi kwa taifa kuelezea jinsi virusi vya corona vilivyoyasambaratisha maisha lakini akiwa na matumaini ya ushindi. 

Takribani hotuba yote nzima imejikita kwenye suala tete nchini Ujerumani na kote ulimwenguni kwa sasa - janga la virusi vya corona, ambapo ameonya kwamba bado janga la maambukizo ya virusi hivyo linaendelea kuwa kitisho kikubwa kwa maisha ya Wajerumani, ingawa amesema kuwa anatiwa moyo kuona jinsi nafsi za watu zilivyojaa umadhubuti mbele ya janga hilo. 

Rais Steinmeier amesema kirusi hicho kiduchu kimechukuwa umiliki wa maisha na fikira za watu, huku kikichafuwa mipango na kuharibu ndoto zao. Mpira kwenye viwanja vya soka, sinema na matamasha ya muziki, safari za likizo, na hata sherehe za harusi, ni miongoni mwa mambo ambayo yaliyokuwa yafanyike ndani ya kipindi hiki, lakini yameshindikana," amesema Rais Steinmeier.

Kiongozi huyo amegusia pia jinsi wanafunzi wanavyokereka na familia zilizofadhaika kutokana na kulazimika kukidhi masharti ya corona kwa kusomea nyumbani na huku wakati huo huo wazazi wakilazimika kuzitunza familia zao.

"Fadhaa pia iko kwa wasanii, wasafishaji, wafanyakazi wa hoteli na wafanyabiashara za rejereja, ambao wanahofia kushindwa kabisa kuyamudu maisha kutokana na kazi zao ambazo zimeathirika sana na janga hili," amesema.


EmoticonEmoticon