Rais wa
Ufaransa Emmanuel Macron amekutwa na virusi vya corona, taarifa kutoka ofisi
yake zimeeleza.
Macron mwenye miaka 42-alifanya vipimo mara tu alipoanza
kujisikia daalili, na sasa anajitenga kwa muda wa siku saba, taarifa kutoka
Ikulu zimeeleza.
Na kuongeza kusema, Bwana Macron bado anaendelea na shughuli
za kuiongoza nchi huku akiwa amejitenga.
Wiki hii, Ufaransa iliweka marufuku ya watu kutotembea muda wa usiku baada ya maambukizi ya corona kuongezeka.
EmoticonEmoticon