Raisi Wa Kenya Na Somali Wakutana Kuzungumza Kwa Pamoja

 

Kulingana na picha zilizochapishwa na Ikulu ya rais nchini Kenya siku ya Jumapili, December 20 , viongozi hao wawili walionekana katika mkutano ambao pia ulihudhuriwa na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na mwenzake wa Sudan Abdalla Hamdok.

Menyekiti wa muungano wa Afrika Moussa Faki Mahamat, ambaye alikuwa mmoja ya wazungumzaji katika mkutano huo alizungumzia kuhusu umuhimu wa kutatua mgogoro kati ya Kenya na Somalia.

''Hali ya wasiwasi ilioshuhudiwa hivi karibuni kati ya Kenya na Somalia inatutia wasiwasi katika muungano huu . Hivyobasi , ningependa kuomba mataifa yote mawili kuanza mazungumzo ili kurudisha uhusiano wa kidiplomasia na ningependekeza IGAD kuunga mkono pendekezo hili'', alisema Moussa.

Taifa la Somalia limekatiza rasmi uhusiano wa kidiplomasia na Kenya huku taifa hilo likiendelea kuilaumu Kenya kwa kujaribu kuingilia uhuru wa taifa hilo kujitawala.


EmoticonEmoticon