Rais wa
Russia Vladmir Putin amesaini sheria inayotoa kinga ya kutoshitakiwa kwa
waliokuwa marais wa nchi hiyo.
Sheria hiyo
vile vile inatoa fursa kwa marais wa zamani kuwa maseneta wa maisha katika
bunge la juu la nchi hiyo, punde tu wanapoondoka madarakani.
Sheria hiyo
inafuatia mabadiliko makubwa ya kisiasa ambayo yamefanywa na Putin nchini
Russia, mwaka huu.
Sheria hiyo
ni sehemu ya mabadiliko ya katiba yaliyopitishwa kote nchini humo mwaka huu, na
kumruhusu Putin kusalia madarakani hadi mwaka 2036.
Alikuwa
anatarajiwa kuondoka madarakani mwaka 2024.
Marais wa
Zamani wa Russia walikuwa tayari na kinga ya kisheria, kutoshitakiwa kutokana
na makosa waliofanya walipokuwa madarakani.
Sheria ya
sasa inatoa kinga ya kutoshitakiwa maisha yao yote, hawawezi kukamatwa,
kukaguliwa, kuchunguzwa wala kufunguliwa mashtaka.
Sheria mpya pia inaweka mazingira magumu kabisa ya kuondoa kinga ya kutoshitakiwa kwa marais wa zamani.
EmoticonEmoticon