Raisi Wa Urusi Asema Nchi Yake Ina Kombora Lisiloweza Kuzuiwa Na Marekani

 

Urusi inamiliki kombora ambalo haliwezi kutunguliwa na linaweza kufika pahala popote duniani, kwa mujibu wa Rais Vladimir Putin.

Amesema kombora "halipai juu sana, ni vigumu sana kulitambua likipita, lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia na linaweza kufika popote pale.

Aidha, njia linayofuata haiwezi kutabirika na adui, linaweza kukwepa vizuizi na kimsingi haliwezi kuzuiwa na mifumo ya sasa ya kinga dhidi ya makombora na hata mifumo inayotarajiwa kuundwa siku zijazo."

Huku akitumia skrini kubwa, alionyesha video za alichosema ni kombora jipya la Urusi. Alisema kombora hilo haliwezi kuzuiwa na mfumo wa kinga wa makombora wa Marekani barani Ulaya na Asia.

Kadhalika, ameonesha video ya ndege isiyo na rubani inayoweza kufanya kazi chini ya bahari.

Kwenye hotuba hiyo yake kwa kikao cha pamoja cha mabunge mawili, aliwahamasisha raia kupendekeza majina ya kupewa mifumo hiyo miwili ya silaha.


EmoticonEmoticon