Rihanna Aripotiwa Kutoka Kimapenzi Na Rapa Asap Rocky

 

Staa wa Muziki duniani Rihanna ameripotiwa kuwa anatoka kimapenzi na rafiki yake wa muda mrefu rapa Aasap Rocky , kwa mujibu wa chanzo cha karibu na wawili hao .

Kwa mujibu wa Jarida la New York Post, limeripoti kwamba wenzi hao wote wawili wenye miaka 32 , walionekana wakila chakula cha jioni na marafiki huko Beatrice Inn huko New York mwishoni mwa wiki hii.

Wawili hao walianza kuhusishwa na uvumi wa mapenzi tangu Rih alipotengana na mpenzi wake wa miaka mitatu, bilionea Hassan Jameel, mnamo Januari.


EmoticonEmoticon