Wanamgambo
wa Islamic State (IS) walijaribu kutengeneza ndege zisizo na rubani zenye kasi,
zinazotumia nguvu ya injini ya jet kama zile zilizotumiwa katika mabomu ya V-1
yaliyodondoshwa Uingereza wakati wa vita ya pili ya dunia , uchunguzi umebaini.
Waangalizi wa masuala ya mizozo , Conflict Armament Research
(CAR) wamebainisha injini kwenye ripoti mpya kuhusu namna gani IS ilipata na
kutengeneza silaha
Tangu mwaka 2014, IS iliweka utawala wake wa kikatili kwa
mamilioni ya watu, walipodhibiti eneo la kilomita za mraba 88,000 la mamlaka
linaloanzia Magharibi mwa Syria kuelekea Mashariki mwa Iraq.
IS walitangazwa kudhibiwa nchini Syria na Iraq mwezi Machi
mwaka 2019.
Baada ya miaka mitano ya mapambano makali, vikosi
vinavyoungwa mkono na Marekani na washirika wake waliweza kurejesha maeneo
yaliyokuwa yakidhibitiwa na IS.
"Hakuna kundi jingine lolote lenye silaha linalofikia
uwezo na uzalishaji wa silaha wa IS,'' Mike Lewis, Mkuu wa taasisi ya CAR
aliyoongoza uchunguzi huo ameeleza.
Namir Shabibi, Mkuu wa shirika la operesheni nchini Iraq, amesema "wanamgambo waliobaki Iraq na Syria wamekuwa machachari katika kipindi cha mwaka uliopita".
EmoticonEmoticon