Seneta Wa Republican Kupinga Kuidhinishwa Kwa Joe Biden

 

Mwanachama wa Republican anasema kwamba atakuwa seneta wa kwanza kupinga wakati bunge la Congress litakapomuidhinisha rais mteule Joe Biden wiki ijayo.

Seneta wa Missouri Josh Hawley alisema kwamba alikuwa na wasiwasi wa maadili licha ya kutokuwa na ushahidi wa kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi uliopita.

Kundi moja la wanachama wa Republican katika bunge wawakiishi pia linapanga kupinga matokeo ya uchaguzi.

Lakini pingamizi hizo hazitarajiwa kubadilisha matokeo. Siku ya kuapishwa kwa rais mteule na makamu wake itakuwa tarehe 20 Januari.


EmoticonEmoticon