Bunduki-ya
setilaiti na "yenye intelijensia bandia" ilitumika kumuua
mwanasayansi mkuu wa nyuklia wa Iran, kamanda wa jeshi la Iran ameeleza.
Mohsen Fakhrizadeh aliuawa kwa kupigwa risasi katika msafara
nje ya Tehran tarehe 27 mwezi Novemba.
Brigedia Jenerali Ali Fadavi aliwaambia wanahabari wa eneo
hilo kuwa silaha hiyo iliyokuwa imewekwa kwenye lori la kubeba mizigo, iliweza
kufyatua risasi huko Fakhrizadeh bila kumpiga mkewe pembeni yake. Madai hayo
hayakuthibitishwa.
Iran imeilaumu Israeli na kundi la upinzani lililohamishwa kwa shambulio hilo.Israel haijakiri wala kukana kuhusika na mashambulizi.
EmoticonEmoticon