Mamlaka ya
Singapore imekuwa nchi ya kwanza duniani kuruhusu nyama ambayo haijatoka kwa
mnyama aliyechinjwa.
Maamuzi hayo yametoa mwanya wa kuanza kuliwa kwa nyama ya
kuku ambayo imetengenezwa katika maabara.
Kampuni ya kutengeneza nyama hizo haijasema zitakuwa tayari
lini kuanza kutumika.
Uhitaji wa nyama mbadala unaongezeka kutokana na wasiwasi wa
wateja juu ya afya zao ,makuzi ya wanyama na mazingira yanayowazunguka.
Kwa mujibu wa Barclays, soko la nyama mbadala itaweza kuwa na
thamani ya dola bilioni 140 (£104bn) ndani ya muongo ujao, au asilimia zipatazo
10 za viwanda vya nyama duniani vyenye thamani ya dola trilioni 1.4tn .
Nyama zinazotegemea mimea zimekuwa na vyakula vingine ambavyo
huwezi kuvidhani vimeongezeka katika maduka makubwa pamoja na migahawa
mbalimbali.
Lakini kula tu hizi bidhaa ni tofauti kwasababu hazina uhusiano wowote na mimea lakini huwa zinakuzwa katika maabara.
EmoticonEmoticon