Serikali ya
Somalia Jumatatu ilisimamisha utoaji wa vibali vinavyotolewa kwenye uwanja wa
ndege nchini humo kwa wageni kutoka Kenya.
Badala yake iliwashauri wote wanaosafiri nchini humo kuomba
Viza kwenye ubalozi wake mjini Nairobi kabla ya kusafiri.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, amri hiyo
itaanza kutekelezwa Decemba 13.
Ofisi ya uhamiaji ya Somalia imesema kuwa hatua hiyo
imepelekewa na tahadhari dhidi ya maambukizi ya Covid19.
Taarifa zinaongeza kusema kuwa watu wenye vyeti vya kusafiria
vya kidiplomasia watahitajika kupata idhini kutoka kwa wizara ya mambo ya
kigeni mjini Mogadishu kabla ya kusafiri nchini humo.
Mwezi Novemba mwaka huu, Somalia ilifungua tena ubalozi wake
mjini Nairobi baada ya kufungwa kwa miaka 10 kufuatia ushindi wa kesi dhidi ya
mwekezaji binafsi aliekuwa ameununua kwa njia ya magendo wakati mapigano
yakiendelea Somalia.
Jengo la ubalozi, lililo eneo la Westlands mjini Nairobi,
lilinunuliwa mwaka wa 1972 na limekuwa likikarabatiwa kwa miaka miwili
iliopita.
Sasa ubalozi huo unatarajiwa kufunguliwa tena ukisimamiwa na balozi wa Somalia nchini Kenya, Mohamoud Ahmed Nur Tarsan.
EmoticonEmoticon