Trump Apinga Mpango Wa Kuwapa Chanjo Maafisa Wa White House

 

Rais wa Mareakani Donald Trump amebadili mpangowa kuwapa chanjo ya corona maafisa wa White House katika siku chache zijazo.

Awali maafisa walisema maafisa wa ngazi ya juu katika utawala wa Trump watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupewa chanjo ya corona, maafisa nchini Marekani wamesema.

Maafisa pia walikuwa wamesema baadhi ya wafanyakazi wa White House wanatarajiwa kupewa chanjo ya Pfizer/BioNTech wiki hii.

Chanjo hiyo inatoa ulinzi wa hadi asilimia 95 dhidi ya Covid-19 ana inaidhinishwa kuwa salama na wadhibiti wa dawa wa Marekani iliyopita Ijumaa.

Dozi milioni tatu za kwanza za chanjo hiyo kwasaba zinasambazwa katika maeneo tofauti katika majimbo yote 50 ya Marekani.


EmoticonEmoticon