Rais wa Marekani anayeondoka, Donald
Trump ametofautiana na waziri wake wa mambo ya kigeni, kwa kudokeza bila kutoa
ushahidi kuwa China na sio Urusi, ndiyo iliyohusika na operesheni ya udukuzi wa
mtandao dhidi ya Marekani.
Katika matamshi yake ya kwanza
kuhusu udukuzi huo, Trump aliandika kwenye mtandao wa Twitter akiwadhihaki
wanaoiangazia Urusi na kupuuzilia mbali mashambulizi hayo, ambayo shirika la
Marekani la usalama wa mitandaoni lilionya kuwa yaliweka kitisho kikubwa kwa
mitandao ya serikali ya kibinafsi.
Trump amesema amefahamishwa kikamilifu kuhusu suala hilo na kuwa kila kitu kimedhibitiwa. Waziri wa Mambo ya Kigeni Mike Pompeo alisema Ijumaa usiku ni wazi kwamba Urusi ilihusika na operesheni hiyo dhidi ya Marekani.
EmoticonEmoticon