Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi nchini Uganda Jaji Simon Mugenyi Byabakama, amesema kwamba
tume hiyo haitasita kumchukulia hatua Rais Yoweri Museveni ambaye ni mgombea
urais kupitia chama cha National Resistance Movement – NRM, endapo hatafuta
sheria za kampeni zilizowekwa na tume.
Kulingana na tume ya
uchaguzi, wagombea wanastahili kuandaa mikutano ya kampeni isiyozidi watu 200,
na lazima wafuate maagizo ya maafisa wa afya ya kukabiliana na janga la virusi
vya Corona.
Maagizo hayo ni pamoja na
kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono, kuvaa barakoa na kutokaribiana.
Museveni amekuwa akifuata
maagizo hayo na kuhutubia wafuasi wake kupitia mitandao ya kijamii na vyombo
vya habari, lakini katika siku mbili zilizopita, amehutubia umati wa watu ambao
hawakufuata maagizo ya afya, katika wilaya za Busia na Bukedi.
“Tutamwandikia barua kumkumbusha kwamba
anastahili kufuata maagizo yetu ili sote tupambane na janga la Covid-19,
maagizo yetu hayana ubaguzi na usimamizi wetu wa kampeni hauna ubaguzi” Byabakama
“Unapoidhinishwa na tume ya uchaguzi kugombea
nafasi yoyote, unakuwa mgombea wetu na lazima ufuate masharti yetu,” Byabakama
“Mwelekeo tuliotoa unatumika kwa kila mgombea. Museveni ni mmoja wao na anastahili kufuata masharti yetu. Kila mgombea anastahili kuhakikisha kwamba wafuasi wake ama mawakala wake wa kampeni wanafuata masharti hayo.” Byabakama
EmoticonEmoticon