Uchaguzi Mpya Kufanyika Israel Huku Serikali Ya Umoja Ikivunjika

 

Israel itafanya uchaguzi wake wa nne katika kipindi cha miaka miwili baada ya vyama vikuu viwili katika serikali ya umoja kushindwa kuheshimu muda wa mwisho wa kutatua mzozo juu ya bajeti ya taifa.

Wapigakura watarejea katika uchaguzi mwezi Machi, miezi 12 tu baada ya awamu ya uchaguzi kufanyika.

Uchaguzi wa awali haukukamilika , na hivyo kusababisha kuundwa kwa serikali nadra ya umoja.

Waziri mkuu Benjamin Netanyahu, ambaye kesi ya madai ya ufisadi inaendelea dhidi yake, ana matumaini ya kurejea madarakani kwa muhula wa sita.

Alikana mashitaka ya uhalifu, ambayo aliyapuuzilia mbali akiyataka kuwa yenye uchochezi wa kisiasa.

Jumanne usiku, bunge la Israeli-Knesset, lilivunjwa moja kwa moja kulinga na sheria baada ya makataa ya mwisho kupita ya kuidhinishwa kwa bajeti ya mwaka 2020.

Jaribio la saa 11 la kuepuka kuvunjwa kwa bunge lilishindwa baada ya muswada wa kurugusu kuongezwa kwa muda wa majadiliano zaidi kupingwa kwa kura, kinyume na ilivyo tarajiwa.


EmoticonEmoticon