Wajumbe wa Umoja wa Ulaya na Uingereza wanakutana Jumapili mjini Brussels katika mazungumzo yanayojaribu kufikia makubaliano ya kibiashara ya baada ya Brexit, huku maswala matatu muhimu yakisalia bado kizungumkuti.
Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen
na waziri mkuu wa Uingereza Borris Johnson walifanya mazungumzo kwa njia ya
simu siku ya Jumamosi na kuwaagiza wajumbe wao kuendelea na mazungumzo katika
jaribo la mwisho la kumaliza tofauti zilizoko.
"Tofauti kubwa bado
zimesalia", walisema viongozi hao katika taarifa ya pamoja baada ya
mazungumzo ya njia ya simu kutathmini uhusiano wa baadae wa Uingereza na Umoja
wa Ulaya.
Pande zote zimekiri kwamba muda unayoyoma wa kufikia makubaliano kabla ya kipindi cha mpito kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.
Viongozi hao wawili wamegusia pia maendeleo yaliyopatikana katika maeneo kadha lakini bado kuna mgawanyiko katika suala la haki za uvuvi.
Jonhson na Von der Leyen wamedai kuwa " hakuna makubaliano
yanayowezekana ikiwa tofauti juu ya masuala matatu muhimu ya utawala, uvuvi na
kanuni za ushindani hayatapatiwa ufumbuzi".
"Hii ni kete ya mwisho ya mchezo", kilisema chanzo kimoja cha Uingereza kilicho karibu na timu ya mazungumzo.
"Kuna mpango mzuri unaofaa kufikiwa ambao utafanya kazi kwa pande zote mbili, lakini hili litatokea endapo tu Umoja wa Ulaya utakuwa tayari kuheshimu kanuni za msingi za uhuru na udhibiti".
EmoticonEmoticon