Uingereza Na Umoja Wa Ulaya Zimefanikiwa Kupata Mkataba Wa Baada Ya Brexit

 

Uingereza na Umoja wa Ulaya wamefanikiwa kupata mkataba wa baada ya Brexit siku chache kabla ya muda wa mwisho uliowekwa kumalizika.

Msemaji wa serikali ya Uingereza amethibitisha taarifa hizo muda mfupi uliopita na kusifu kuwa hizo ni habari njema kwa familia na wafanyabiashara nchini humo. 

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen wanatarajiwa muda mchache unaokuja kuweka wazi vipengele vya mkataba huo uliopatikana baada ya mazungumzo ya miezi 10.

Katika kipindi hicho kila upande ulijaribu kuhakikisha mkataba unaofikiwa, utafanikisha usawa kwenye shughuli za biashara baina ya Uingereza na Umoja wa Ulaya baada ya Brexit.


EmoticonEmoticon