Uingereza Yaanza Mpango Wake Wa Utoaji Chanjo Ya COVID-19 Kwa Umma

 

Chanjo ya kinga dhidi ya virusi vya corona ambayo imetengenezwa na kampuni ya Kimarekani ya Pfizer na ile ya Kijerumani BioNTech kwa wakati huu inasambazwa katika hospitali tofauti nchini Uingereza. 

Hatua hiyo inatekelezwa siku mbili kabla ya kuanza kile kinachotajwa kuwa programu kubwa ya zoezi la utoaji chanjo nchini humo. Kiasi cha dozi 800,000 za chanjo zinatarajiwa kuwa kila mahali, kabla ya kuanza utekelezaji wa utoaji wa chanjo hizo hapo Jumanne. 

Mkurugenzi wa tiba wa Uingereza, Profesa Stephen Powis amesema pamoja na changamoto kubwa lakini vituo vya afya kwa sehemu kubwa vitaanza duru ya mwanzo ya utoaji wa chanjo kama ilivyopangwa. 

Juma lililopita Uingereza, lilikuwa taifa kwanza kuridhia matumizi ya dharura chanjo ya Pfizer na BioNtech. Katika majaribio yake chanjo hiyo ilionesha ufanisi kwa asilimia 95.


EmoticonEmoticon