Mkuu wa wafanyakazi wa serikali ya shirikisho ya Ujerumani, Helge Braun amesema hatua ya kuzifunga shughuli za umma nchini humo huenda zisiondolewe Januari 10.
Helge amekiambia siku ya Jumataztu
kituo cha televisheni cha RTL/ntv kwamba ana matumaini hatua kali zilizowekwa
kuzuia kusambaa kwa visa vya virusi vya corona zitasaidia kupunguza maambukizi
Ujerumani.
Amesema
wakati huu wa msimu wa baridi, Ujerumani itashuhudia siku ngumu, ikizingatiwa
kwamba bado chanjo ya virusi vya corona haijaanza kutumika humu nchini.
Kiongozi huyo wa wafanyakazi katika ofisi ya Kansela Angela Merkel amerudia kusema kuwa maduka, shule na vituo vya kuwaangalia watoto vitafungwa kuanzia Jumatano, ikiwa ni katika kuchukua hatua kali za kujaribu kudhibiti ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.
EmoticonEmoticon