Ujerumani Yapiga Marufuku Maandamano Ya Kupinga Vizuizi Vya Corona

 

Polisi katika mji wa kaskazini mwa Ujerumani wa Bremen hapo jana imezima maandamano ya kupinga vizuizi vilivyowekwa na serikali kuzuia kuenea kwa virusi vya corona. 

Maandamano hayo yalifanywa licha ya marufuku iliyotangazwa na mahakama ya juu nchini. Mamia ya raia walikusanyika karibu na kituo kikuu cha treni mjini humo hapo jana majira ya mchana na jioni. 

Maandamano hayo yalihusisha makundi mawili ya waandamanaji, wale wanaopinga vizuizi vya serikali na wale wanaowapinga. Polisi wamesema maafisa wawili wamejeruhiwa. 

Mapema hapo jana, Mahakama Kuu ya Kikatiba ya Ujerumani ilitoa amri ya kuyapiga marufuku maandamano hayo.


EmoticonEmoticon