Raia wa
kusini mwa Madagascar wanakula mchanga uliochanganywa na ukwaju kwasababu ya
kiangazi ambacho kimeharibu zao linalotegemewa na wenyeji, kwa mujibu wa
shirika la habari la AFP.
"Tunauita udongo wenye kuhimili
kiangazi kwasababu unaruhusu ukwaju kukua na kutusaidia kukabiliana na
kiangazi," AFP imemnukuu mkulima wa eneo Doday Fandilava Noelisona.
"Siku hizi hatutafuti tena
chakula bali tunatafuta mbinu za kupata kitu chochote cha kushikilia
tumbo."
Matunda ya dungusi ambayo watu
huyategemea yamekauka kwasababu ya ukosefu wa mvua.
Aidha, shirika la AFP limemnukuu
mkulima mwingine, Avianay Idamy, ambaye anasema amegeukia uuzaji wa makaa
kupata pesa za kukidhi mahitaji ya familia yake angalau waweze kula muhogo mara
moja tu kwa siku.
Shirika la chakula dunia- WFP, linasema watu milioni 1.5 kusini mwa Madagascar wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.
EmoticonEmoticon