Mataifa ya Ulaya yanaanza kutoa chanjo ya virusi vya corona kwa makundi yaliyo hatarini huku aina mpya ya kirusi hicho ikisambaa kwa kasi na Shirika la Afya Duniani likionya kwamba janga la sasa halitakuwa na mwisho.
Dozi za kwanza za chanjo ya Pfizer-BioNTech ziliwasili
kwenye mataifa ya Umoja wa Ulaya zikiwemo Italia, Uhispania na Ufaransa ambazo
zimeathiriwa vibaya na virusi vya corona, tayari kwa ajili ya kusambazwa kwenye
majumba ya kuwatunzia wazee na kwa wafanyakazi wa huduma za afya.
Kuthibitishwa
kwa chanjo hiyo kumeongeza matumani kwamba mwaka 2021 unaweza kuleta ahuweni
dhidi ya janga la COVID-19, ambalo hadi sasa limeshaangamiza maisha ya watu
milioni 1.7 tangu liibuke nchini China mwaka jana.
Chanjo kwenye mataifa yote 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya zimepangwa kuanza kutolewa leo (Jumapili, 27 Disemba), baada ya mamlaka kuiidhinisha chanjo hiyo ya Pfizer-BioNTech tarehe 21 Disemba.
EmoticonEmoticon