Ulaya Yaimarisha Vizuizi Vya Kudhibiti Virusi Wakati Idadi Ikipanda

 

Nchi kadhaa za Ulaya zimeimarisha vizuizi vya kudhibiti maambukizi ya corona, wakati Ujerumani ikiweka rekodi ya vifo vingi kwa siku moja nayo Marekani ikivunja rekodi yake yenyewe ya idadi kubwa ya maambukizi kwa siku. 

Hatua hizo kali zimekuja wakati nchi za Umoja wa Ulaya zikikubaliana kuanza utoaji wa chanjo kwa wakati mmoja. Shinikizo limekuwa likizidi katika jumuiya hiyo tangu Uingereza na Marekani zilipoanzisha mipango yao, zikitumia chanjo iliyotengenezwa katika Umoja wa Ulaya na kampuni za Pfizer na BioNTech.

 Ujerumani imeyafunga maduka yote yasiyokuwa muhimu na shule wakati idadi ya vifo kwa siku moja ikipanda hadi 952. 

Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO tawi la Ulaya limeonya kuhusu kuongezeka kwa maambukizi barani humo hadi mapema mwaka ujao, na kuhimiza kuchukuliwa tahadhari maalum, katika msimu huu wa sherehe. 

Uingereza, Uhispania, Ufaransa, Denmark, Uturuki na Uholanzi zote zimeimarisha vizuizi vyao vya corona.


EmoticonEmoticon