Umoja Wa Ulaya Na Uingereza Wajadiliana Kuhusu Brexit Na Covid-19

 

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson wamezungumza kwa njia ya simu juu ya mkwamo kuhusu masuala ya uvuvi pamoja na kadhia la janga la virusi vya Corona.

Vyanzo vya Umoja wa Ulaya vimesema kuwa Umoja huo uko tayari kukubali punguzo la thamani ya samaki wake katika maji ya Uingereza kwa hadi asilimia 23 katika kipindi cha muda kuanzia mwaka 2021.

Masuala ambayo yamesababisha mkwamo katika mazungumzo hayo ni kiwango cha ushindani sawa na haki za uvuvi zikiwa zimesalia siku tisa pekee kabla ya Uingereza kuondoka kabisa katika Umoja huo.

Hayo yanatokea katika wakati ambapo Ulaya pamoja na mataifa mengine yamesimamisha ndege za abiria kutoka Uingereza ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona baada ya Uingereza kuripoti aina mpya ya kirusi cha Corona chenye kusambaa kwa kasi zaidi.


EmoticonEmoticon