Umoja Wa Ulaya Walegeza Marufuku Za Safari Kuhusu Kirusi Kipya Uingereza

 

Mataifa kadhaa ya Ulaya yameanza kulegeza marufuku ya safari yaliyokuwa yameiwekea Uingereza katika juhudi za kukabiliana na kuenea kwa aina mpya ya kirusi cha corona wakati maafisa wa Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO wakitazamiwa kulijadili suala hilo. 

Kirusi kipya cha corona kimeikumba Uingereza na kuibua wasiwasi duniani kote wakati chanjo ya COVID-19 ikianza kutolewa. Lakini Halmashauri Kuu ya Ulaya imeyataka mataifa ya Ulaya kuondoa marufuku ya safari iliyowekwa dhidi ya Uingereza katika siku za hivi karibuni. 

Ufaransa imeanza kuifungua mipaka yake na Uingereza hii leo, ingawa vipimo kwa ajili ya COVID-19 vitahitajika. Uholanzi nayo imetangaza kuondoa marufuku hiyo, lakini sio kwa abiria wote. 

Nchini Marekani Rais Donald Trump ameukataa mpango mkubwa wa misaada ya kiuchumi ya COVID-19 uliopitishwa na bunge, akiutaja kuwa ni 'fedheha', ikiwa ni chini ya mwezi mmoja kabla ya kuondoka madarakani na wakati mamalioni ya Wamarekani wakiendelea kukabiliwa na janga la corona.


EmoticonEmoticon