Urusi Yadai Mpinzani Wa Serikali Ya Rais Putin Ameathirika Kisaikolojia

 

Ikulu ya Urusi imesema kiongozi wa upinzani Alexei Navalny alikuwa ni “mgonjwa” aliyeathirika kisaikolojia, baada ya kudai kuwa majasusi wa Urusi walimtilia sumu. 

Msemaji wa Rais Vladimir Putin, Dmitry Peskov, amesema kuwa Navalny mwenye umri wa miaka 44 ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali anaumwa maradhi yanayohusiana na hamu yake ya kutaka madaraka. 

Navalny alidai kuwa majasusi wa Urusi ndio waliohusika katika jaribilio la kutaka kumuua kwa kumtilia sumu mnamo mwezi Agosti, tukio ambalo limepelekea Umoja wa Ulaya kuwawekewa vikwazo baadhi ya maafisa waandamizi wa Urusi.

Hata hivyo, idara ya ujasusi ya Urusi ya FSB imekanusha madai yaliyotolewa na Navalny na kuyataja kama yasiyokuwa na ukweli wowote. Idara hiyo imemshtumu Navalny kwa kupokea msaada kutoka mashirika ya kigeni ya kijasusi.


EmoticonEmoticon