Urusi Yafungua Uchunguzi Mpya Wa Jinai Dhidi Ya Navalny

 

Wachunguzi wa umma nchini Urusi wamesema wamefungua mashtaka mapya ya jinai dhidi ya Alexei Navalny ambaye ni mkosoaji mkubwa wa serikali nchini humo. 

Wapelelezi hao wanamtuhumu Navalny na washirika wake ambao hawakutajwa, kwa kutumia dola milioni 4.81 kwa mahitaji binafsi ilhali ni misaada ya umma kwa mashirika anayosimamia.

Hatua hiyo huenda ikatizamwa kama ishara ya hivi karibuni ya Urusi kutomtaka Navalny ambaye anaendelea kupona nchini Ujerumani baada ya jaribio la kuuawa kwa kuwekewa sumu mwezi Agosti.

Navalny ni miongoni mwa wakosoaji wakubwa wa rais wa Urusi Vladimir Putin. Hata hivyo Urusi ambayo imepinga madai ya kumtilia Navalny sumu, imesema yuko huru kurejea nyumbani, jambo ambalo mwenyewe amekiri anapanga kufanya.


EmoticonEmoticon