Utafiti: Idadi Kubwa Ya Watu Kutopata Chanjo Ya COVID-19 Hadi 2022

 

Utafiti mpya uliotolewa leo unaonesha idadi kubwa ya watu duniani haitaweza kupata chanjo ya Covid-19 hadi 2022, huku kwa mataifa tajiri kukiwa na uwezekano wa zaidi ya nusu kuipata katika nusu ya mwanzo ya 2021. 

Katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na matumaini kwamba chanjo hiyo inaweza kuzuia janga hilo ambalo limesababisha vifo vya takribani watu milioni 1.6, mataifa kama Marekani, Uingereza na Umoja wa Falme za Kiarabu yameanza programu za utoaji wa chanjo wa kwa watu wake. 

Na bado yapo katika jitihada ya kutanua zaidi huduma hiyo katika maeneo tofauti ya mataifa yao.

Utafiti wa asasi yenye kujikita katika masuala ya afya ya John Hopkins Bloomberg unaonesha mataifa tajairi ambayo yanafanya jumla ya asilimia 14 ya idadi wote duniani yameagiza zaidi ya nusu ya dozi ya chanjo ambayo itarajaiwa kuzalishwa na makampuni 13 hadi mwaka ujao.


EmoticonEmoticon