Viongozi Wa EU Wamaliza Mvutano Kuhusu Bajeti

 

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano kuhusu bajeti ya muda mrefu na mpango wa uokozi wa uchumi baada ya wiki kadhaa za upinzani kutoka mataifa mawili wanachama ya Poland na Hungary. 

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mkutano wa kilele wa viongozi wakuu wa Umoja wa Ulaya unaoendelea mjini Brussels.

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya Charles Michel amesifu hatua iliyofikiwana kusema inatoa nafasi ya kuanza utekelezaji wa bajeti ya kanda hiyo pamoja na kuimarisha tena chumi za mataifa wanachama chini ya mpango wa uokozi unaolenga kufufua shughuli za uzalishaji baada ya janga la virusi vya corona.

Hungary na Poland zilitumia kura ya turufu kuzuia kupitishwa kwa bajeti ya dola Trilioni 1.3na mpango wa uokozi wa dola bilioni 900 kufuatia masharti kuwa utolewaji wa fedha hizo ungezingatia jinsi nchi wanachama zinavyozingatia misingi ya utawala sheria na demokrasia.

Masharti hayo yangeruhusu kuzuiwa nchi mwanachama kupatiwa fedha pindi misingi kadhaa ya demokrasia na utawala wa sheria itakiukwa ikiwemo uhuru wa mahakama au kukosekana uadilifu katika usimamizi wa bajeti.


EmoticonEmoticon