Viongozi wa Iran: Kuingia Kwa Biden Hakumaanishi Mahusiano Bora Ya Haraka

 

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na rais wa nchi hiyo Hassan Rouhani wameionya Marekani kuwa kuondoka kwa Rais Donald Trump hakumaanishi kuwa mahusiano kati ya mataifa hayo mawili yataboreka haraka. 

Akizungumza mjini Tehran Khamenei aliuambia mkutano wa viongozi waandimizi wa kijeshi kuwa Marekani chini ya Trump na mtangulizi wake 

Barack Obama ilikuwa na uhasama dhidi ya watu na taifa la Iran. Rouhani, akizungumza katika baraza la mawaziri, alimkosoa Trump na hata kusema kuwa rais huyo wa Marekani wakati mmoja alifanya uhalifu mwingi, alikuwa muuwaji na gaidi. 

Alisema Iran haina furaha sana kuwa Joe Biden anaingia madarakani, na ina furaha kubwa kuwa Trump anaondoka. 

Matamshi hayo yamekuja wakati Iran ikikaribia kufanya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu shambulizi la ndege ya Marekani isiyoruka na rubani lililomuua kiongozi wa Jeshi la Mapinduzi jenerali Qassem Soleimani mjini Baghdad, shambulizi ambalo karibu lizitumbukize Marekani na Iran katika vita baada ya mivutano.


EmoticonEmoticon