Rais wa
Pakistan amesaini sheria mpya itakayotoa adhabu kali dhidi ya wahusika wa
ubakaji.
Kulingana na sheria hii , serikali itaweka sajiri ya watu
wanaopatikana na makosa ya ubakaji, kulinda utambulisho wa waathiriwa na
matumizi ya kemikali kuwahasi baadhi ya wabakaji.
Kulingana na sheria hii, kesi za ubakaji zitaharakishwa.
Mahakama zinatarajiwa kukamilisha kesi ya ubakaji ndani ya kipindi cha miezi
minne.
Serikali imesaini sheria mpya dhidi ya ubakaji baada ya
malalamiko megi ya watu dhidi ya unyanyasaji huo wa kingoni baada ya wanaume
kadhaa kumbaka mwanamke mmoja nje ya jiji la Lahore.
Walimbaka mwanamke huyo kando ya barabara inayoelekea katika
jiji hilo mbele ya watoto wake wawili. Mkuu wa polisi alisema kuwa muathiriwa
kwa upande mmoja alikuwa na makosa.
Kauli yake
pamoja na unyanyasaji huo wa kinyama viliwakasirisha watu nchini humo ambao
walisema kuwa amegeuza ukatili huo kuwa kitu kidogo. Maandamano makubwa
yamekuwa yakiendelea kuilazimisha serikali kuchukua hatua dhidi ya ubakaji.
Waziri Mkuu Imran Khan na baraza lake la mawaziri
waliidhinisha sheria hiyo na Rais Arif Alvi akaisain kuwa sheria Jumanne.
Serikali ilipewa siku 120 na umma kuwa imeidhinisha sheria hiyo na kupitishwa na bunge.
EmoticonEmoticon