Japan
inapanga kuinua kiwango chake cha uzazi wa watoto kinachopungua kwa ufadhili
intelijensia bandia ya mfumo wa kufananisha ili kuwasaidia wakazi kuwapata
wapenzi.
Kuanzia mwaka ujao serikali ya nchi hiyo itazisaidia serikali
za majimbo ambazo tayari zimeanza kuendesha mfumo huo au kuanzisha miradi
ambayo inatumia Intelijensia bandia kuwakutanisha watu.
Mwaka jana idadi ya watoto wachanga waliozaliwa nchini Japan
ilishuka chini ya 865,000 - ikiwa ni rekodi ya chini kuwahi kushuhudiwa.
Nchi hiyo ambayo ina idadi kubwa ya watu wanaozeeka kwa
haraka kwa muda mrefu imekuwa ikitafuta njia za kupunguza viwango vya chini
zaidi vya uzazi duniani vinavyoshuhudiwa katika taifa hilo.
Kuongeza
matumizi ya teknolojia ya Intelijensia bandia (IT) ni moja ya juhudi zake za
hivi karibuni kujaribu kukabiliana na tatizo hilo.
Mwaka ujao serikali inapanga kuzitendea mamlaka nchini humo yen bilioni 2 (dola milioni 19 ) ili kuinua kiwango cha uzazi , limeripoti shirika la habari la AFP.
EmoticonEmoticon